The best and the brightest students shouldn't be denied access to higher education simply because they can't afford it~Bill Gates
_________________
If you can't fly, run; if you can't run, walk; if you can't walk, crawl; but by all means keep moving~Dr. King
_________________
When leaders sacrifice the long-term welfare of society for personal or political short-term benefits, then you are on the road to violence and state failure~Dr. Brian Cooksey
_________________
Some men see things as they are and say, 'why?' I dream things that never were and ask, 'why not?'~RFK
_________________
Intellectuals solve problems; geniuses prevent them~ Albert Einstein.
Siku moja Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mhe. Ameir akifuatana na Mhe. Maokola Majogo walikuja Butiama bila taarifa. Walipofika nilikwenda kumwita Mwalimu shambani na njiani alisema kwa masikitiko kwa nini nilichelewa kumpa taarifa kuhusu ujio wa wakubwa hao. Nilimwambia wamekuja ghafla. Kabla ya kuwasalimu Mwalimu alikwenda kusali chumbani kwake na alipotokea aliwauliza kuna jambo gani kubwa ambalo liliwaleta pasipo taarifa. Walijibu kuwa wametumwa na Kamati kuu ya CCM kumweleza kuwa anaaibisha CHAMA kwa kuzungumza na wapinzani Mrema na Sharif. Mwalimu aliuliza walikuja kwa njia gani? Wakajibu kuwa kwa ndege. Akauliza ndege gani? Wakajibu Jet ya Rais. Akauliza tena: ile ambayo nilikuwa natumia? Wakasema ndiyo! Mwalimu aliuliza hivi mnapo niita Baba wa Taifa nilileta maombi (application) serikalini au katika chama niitwe hivyo? Hivi Mrema na Sharif siyo watanzania? Hivi kuunda vyama vya upinzani ni usaliti? Hivi nyinyi CCM kama hamnihitaji kwa ushauri kwa vile mnajua kila kitu basi nisizungumze na vyama vingine? Hivi hamjui kuwa mimi Baba wa Taifa ni above political parties? Mmesema nina kadi namba moja, sawa kwa hiyo mmekuja kunikamata hapa kwetu nilipozaliwa? Maana wewe Ameir ni Waziri wa Mambo ya Ndani na Majogo Ulinzi? Aliendelea kwa kusema kuwa, kama hilo ndilo lililowaleta na kama mmetumwa na mwenyekiti Mhe. Ali Hassani Mwinyi na kamati yake ya Central Commitee (CC) basi kuleni chakula na baada ya hapo nitawapa kadi yenu kisha ondokeni! Mimi naijali na kuipenda Tanzania kuliko vyama vyenu, mnasikia?...[Habari Kamili >>]
Mfano hai wenyewe uko hivi: Mara baada ya kurudi Butiama, 1995, baada ya kuenguliwa kugombea nafasi ya urais, siku moja mapema asubuhi Bwana Lowasa alinipigia simu na kusema yafuatayo: “Bwana Kasori, naomba uende kumwambia Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aende Monduli kusaidia kusafisha jina langu ili nisikose ubunge kutokana na yale aliyonisema Dodoma”. Nilishikilia mkono wa simu (TTCL) kwa zaidi ya nusu saa tukiwa tunazungumza na hatimaye mimi nilipata ujasiri wa kumwambia Bwana Lowasa kuwa siwezi kwenda kusema maneno hayo kwa Baba wa taifa na kwamba akitaka aje Butiama na nitamruhusu waongee ana kwa ana. Nikanyamaza na hatimaye yeye akawa wa kwanza kukata simu. Hiyo ikawa itifaki njema kwangu! Kesho yake tena asubuhi nilipokea simu, safari hii akawa ni mheshimiwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Kwa maneno yake alisema “Bwana Kasori, jana ulizungumza na Edward Lowasa; naomba ufikishe ombi lake kwa Baba wa taifa tafadhali.” Kutokana na heshima ya Mheshimiwa Mzee Kawawa, nilikubali na nikaenda na kabla ya hapo nilimuomba Mzee Kawawa akae karibu na simu ili nimpe jibu muda si mrefu. Nilimueleza Baba wa Taifa kuwa “Mheshimiwa Edward Lowasa kupitia kwa Mhe. Mzee Rashidi Mfaume Kawawa anaomba usaidie kusafisha jina lake kule jimboni kwake Monduli ili asikose ubunge kutokana na yale uliyomsema katika Kamati Kuu ya CCM Dodoma”. Jibu la Baba wa Taifa alilonipa ni kuwa “Nenda umwambie Mzee Rashidi Mfaume Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa!” Ningependa...[Habari Kamili >>]
Baada ya wandamanaji wengine wote kuwa wamenyamazishwa tuli na zaidi ya watu mia saba wakiwa wameripotiwa kuuawa, picha ya shujaa mwenye shati jeupe na suruali nyeusi akiwa amesimama peke yake mbele ya sanjari ya vifaru vya kijeshi vilivyokuwa vikiviringika kuelekea kwenye viwanja vya Tiananmen kuwatawanya wanafunzi-wandamanaji itabaki kuwa na sehemu ya pekee kila mara siku ya kihistroria ya jumatatu June 4, 1989 itakapokumbukwa. Wang Weilin ni jina bandia alilopewa Rais mstaafu Jiang-Zemin (kipindi hicho katibu mkuu wa CCP) alipotaka kujua zaidi kuhusu mwandamanaji huyo. Lakini ukweli ni kwamba, hadi leo hii hakuna anayefahamu jina lake halisi kiasi cha kupelekea abatizwe jina bandia--"The Tank Man".
"The Tank man" anatukumbusha kuwa mchakato wa mabadiliko yoyote yale yawe ya kisiasa, kijamii ama kiuchumi hayataletwa na viongozi wenye majina makubwa yaliyozoeleka masikioni mwetu (Malecela, Kingunge, Malima, Mwinyi, Chambiri, Msuya, Sitta); bali mabadiliko halisi yataletwa na raia wa kawaida watakaohiyari kujitoa mhanga ili kutetea maslahi ya taifa bila kujali yatakayowakumba apo baadaye. Kama Rais Kennedy alivyowahi kusema, nami namnkuu: "utu wa kweli umekamilika ndani ya yule anayediriki kufanya kila awezacho kutetea haki na uhuru wake pasipokujali madhara yanayoweza kumkumba hapo baadaye." Yumkini kitu hichohicho ambacho mwanafalsafa Lao Tzu alikiita "The Tao" (virtue), ndicho pia kilichowasukuma wanaharakati wa miaka ya sitini (1960s) kama vile Martin Luther King Jr, Ho Chi Minh, Patrice Lumumba, na wengine wengi kusimama kidete na kupinga vitendo vya udhalimu na uonevu vilivyokuwa vikiendeshwa na kundi la watu wachache waliodhani kuwa wanayohaki ya kufanya kila walichojisikia kufanya pasipo kuulizwa ama kuzuiliwa na mtu yoyote yule...[Habari Kamili >>]