Barua za Wazi:

 

 

KAMA NINGEKUWA RAIS WA TANZANIA

Kwa Katika makala zangu zilizopita, nimesisitiza haja ya wananchi kuwa na fikara huru (free minds) ili kujiletea maendeleo yao. Nimesisitiza pia haja ya wananchi kuacha tabia ya kuomba misaada au kubweteka huku wakisubiria serikali za nje ziwaletee maendeleo. Nimesisitiza pia haja ya vijana kuacha kukaa vijiweni huku wakisubiri viongozi wao wa serikali wawaletee maendeleo. Naomba msomaji uendelee kutambua kuwa bado sijabadili msimamo huu na sio nia ya makala hii kumtaka Raisi wa nchi atuletee maendeleo. Swali la msingi hapa ni kuwa; je ni kwa kiwango gani Raisi wa nchi anakubaliana na ukweli kuwa serikali ya nchi inaajiriwa na wapiga kura wa nchi hiyo? Ni kwa kiwango gani viongozi wengine wa serikali wanautambua ukweli kuwa wameajiriwa na wapiga kura na walipa kodi? Nikiwa bado natafuta maswali ya majibu haya, nimeamua kuanzisha mjadala mwingine kichwani mwangu. Ninaisumbua akili yangu ijibu swali kuwa; kama mimi ningekuwa Raisi wa Tanzania, je ningeifanyia nini nchi yangu na wapiga kura walioniajiri kuwaongoza?..... [Habari kamili>]

USHAURI KWA VIONGOZI WA SERIKALI--AWAMU YA NNE

Nianze kwa kusema mimi ni mtumishi mstaafu niliyekuwa nimeajiriwa na serikali ya Tanzania kuanzia tarehe 01.01.1969 hadi tarehe 02.06.2005. Ngazi ya juu niliyofikia ni kubahatika kuwa katibu ( msaidizi mkuu kiserikali ) wa Mwalimu J.K Nyerere: Fedha zilizoporwa na tulizopoteza kupitia mikataba mibovu zimeua/zimedhoofisha asilimia kubwa tu ya watoto wetu waliostahili kupata elimu nzuri/bora hapa nchini. Fedha hizo kama walivyokwisha sema waandishi wa habari (tunaowadharau na kuhujumu juhudi zao na kusifia waandishi wa nje) zingesaidia kuboresha majengo ya vyuo vikuu vya mlimani (DSM), Muhimbili na Sokoine. Hali ilivyo sasa mlimani, binafsi naona aibu kusema kuwa nilisoma hapo! Kwa taarifa yenu yale majengo ya awali ya mlimani yalikuwa na hadhi ya kimataifa ikiwa ni pamoja na chakula tulichokuwa tunapata kama wanafunzi. Hata Baba wa Taifa ilikuwa ni kawaida yake kuja kushiriki nasi katika chakula cha jioni kila mwaka-ANNUAL DINNER! Pia ilikuwa ni kawaida yake mara nyingi kuja kuzungumza nasi (siyo kutuhutubia na kufoka)...[Habari Kamili >]

MWAKA UMEISHA SERIKALI IMEFANYA NINI?

Kwakweli kuchaguliwa kwa Rais Kikwete kulitupatia watanzania matumaini mapya. matumaini ambayo labda tulikuwa tumeshayapoteza muda mrefu au hatukuwahi kuwa nayo hapo awali.  Lakini yeye, serikali yake na chama chake hasa ilani yao ya uchaguzi, ilitoa ahadi nyingi ambazo kama zikitekelezwa zitafanya taifa lipige hatua kubwa. Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 iliahidi kuboresha maisha ya watanzania na kuwaletea maendeleo katika kila nyanja ya maisha yaani kiuchumi, kijamii na kisiasa. Rais na chama chake waliahidi kuboresha huduma za jamii kama shule, hospitali, barabara, huduma za maji n.k. Lakini kwa walala hoi wengi, labda ahadi kubwa tunayoikumbuka ambayo mheshimiwa Rais aliitoa wakati wa kampeni na katika hotuba yake wakati wa kuapishwa ni ile ya kuleta nafasi mpya za kazi zipatazo milioni moja katika awamu yake ya kwanza ya uongozi. Lakini zimo nyingine nyingi alizotoa wakati wa kampeni na katika siku za kwanza za uongozi wake likiwemo tatizo kubwa la umeme na pia kero za Muungano. Kuna swala la mikataba isiyonufaisha nchi na wananchi ambayo pia aliahidi itapitiwa na kubadilishwa kama.....[Habari Kamili >>]

Linux web hosting - Get rock solid web hosting at Webquarry!

www.bongotz.com ©Copyright:BongoTz.Com -MMV. All Rights Reserved.