Kona ya Bongo Mchicha:

KARIBUNI, "KONA YA BONGO MCHICHA!!

Ahlan Wasahlan Muhaligani wapendwa wasomaji wangu karibuni mjumuike nami katika Kona hii Murua ya Bongo Mchicha ili kuweza kupata haya na yale kuhusiana na masuala ya mbalimbali ya kijamii,kisiasa na kiutamaduni kupitia Mtandao huu wa bongotz. Hii ni pamoja na mambo mbalimbali yaliyojiri na kuchomoza duniani, Afrika, Afrika Mashariki, na hususan nyumbani Tanzania (Bongo).Jina langu ni Antar Sangali. Kitaaluma mimi ni Mwandishi wa Habari na Mtangazaji katika Radio Uhuru ya Jijini Dar es Salaam.Mwenyeji na Mkaazi wa Bagamoyo Mkoani Pwani kwa ufupi nina uzoefu wa muda mrefu katika uandishi wa Habari na kufanya kazi za Siasa kwa miaka kadhaa. Nathubutu kusema ni mwanasiasa chipukizi niliyechoshwa haraka na siasa pinzani za Tanzania na sasa nimeaumua kuabudu dini yangu na kufanya kazi za taaluma nilionayo.Ikibidi waweza kuwasiliana nami kwa
kunitumia barua pepe za maoni mbalimbali na kunitanabahisha kupitia antabo2@hotmail.com au antarsangali@yahoo.co.uk

BONGO NA ULAYA SAWA TU!

...Kama ni 'Skyscrapers' --bongo zipo..., 'Subway' hazihesabiki...,' Shopping Mall' (walahi bilai) ziko kila kona..; kwanini sasa hutaki kurudi nyumbani...? Ha...ha...ha! kama leo Remmy angetunga wimbo mpya kuhusu "Kurudi nyumbani"--Huenda pengine angetumia maneno ya hapo juu ili kupenyeza ujumbe wake kiurahisi ndani ya akili za vijana wa kitanzania waliozamia majuu na ambao bado wana dhana potofu kuwa bongo yasasa na ile ya miaka ya "arobaini na saba" zote ni sawa. Ndugu msomaji, kama huamini kuwa bongo ya sasa haina tofauti kubwa sana na majiji makubwa ya dunia ya kwanza, hebu angalia viambatanisho vifuatavyo....[Hapa>]

MFUMO WA UCHAGUZI ZANZIBAR UBADILISHWE

Ili kuepuka utata na kuweka mazingira bora ya kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki visiwani, hatimaye kila pande kisiasa ziridhike na matokeo, kuna kila haja yalazima Zanzibar kuiga mfumo wa uchaguzi wa Israel. Kimsingi chaguzi zote zilizofanyika Zanzibar toka mwaka 1957, 1961 , 1961,1963 na baadaye 1995 na 2000 : nidhahiri historia imekuwa ikijirudia kila miongo inavyozidi kupita katika siasa za Visiwa hivyo na kuibua malalamiko na shutuma toka upande mmoja wa siasa dhidi ya mwingine...[Habari Kamili>>]

 

©Copyright: BongoTz.Com-MMV. All Rights Reserved