WASEMAVYO WANANCHI KUHUSIANA NA MSHITO WA DARWIN'S NIGHTMARE
Na, <Mhariri mkuu >
Kufuatia makala ya tarehe 04/08/06 iliyochapishwa na tovuti hii kuhusiana na filamu ya [Darwin's Nightmare], tumepokea maoni mbalimbali toka kwa watanzania waishio nje na ndani ya nchi, na hivi ndivyo walivyosema....
"...Binafsi nimeishi Mwanza kwa takriban miaka sita, katika kipindi hicho hicho makala hiyo ilipoandaliwa na Bwana Sauper. Ukweli ni kwamba Mfaransa huyo anahitaji kupongezwa kwa filamu hiyo ambayo binafsi naweza kushadadia kwa kusema kwamba yote ni ukweli tena ukweli mtupu kwa sababu zifuatazo: Swala la minofu ya samaki sio siri kabisa na kwanza hata mimi na wenzangu hatukuwa tukijua kwamba kula mapanki ni kashfa kwani ni jambo la kawaida sana kwa watu wa hali ya chini huko mwanza, ukizingatia hali ya maisha ya wanunuaji na bei ya mapanki wachuuzi hawawezi hata kidogo kuyahifadhi katika sehemu bora kama majokofu hivyo hutunzwa kwa kuanikwa juani sehemu ya wazi. Now, tell me itachukua muda gani kabla hayajaharibika, ndani ya masaa 3 hadi 4. Ukahaba katika mialo (sehemu wanakipumzikia wavuvi baada ya kazi) katika mwalo mmoja sehemu za Magu niliwahi kushuhudia wanawake wakiitwa wasimbe ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kuwapikia wavuvi chakula na kuwastarehesha kingono na rafiki yangu mmoja kutoka sehemu za ukerewe akaniambia hilo ni jambo la kawaida hata kule kwao wapo tena wengi tu na mwingine kutoka kisorya- Bunda akamuunga mkono. Achilia mbali makahaba waliojaa katika madanguro yao Mwanza mjini na viungani mwake. Mwaka jana mwezi wa June nilikuwa Semina hapo Mwanza na kubahatika kuingia katika moja ya madanguro hayo hapo kirumba, its just like a Studio ya kuuza kanda lakini ukiingia humo ndani utakavyochangamkiwa utashangaa kisha kaduka kadogo wauzaji wengiiii halafu wamejipamba acha mchezo.. I can not prove swala zima la silaha but in a normal common sense wapiganaji wa kongo-Kinshasa, Sierra Leone, Rwanda , Burundi, Uganda, Sudan na hata Somalia achilia mbali angola na Msumbiji wanaishi Msituni for over 10 years fighting! Silaha wanapata wapi? achiliambali mishahara na chakula kwa muda wote huo. You don't need a degree kuliona na kulielewa hili! Sijui kama Rais halioni..." [Matiko. S. --DSM, Tanzania]
"...Nini cha ajabu ambacho Mr. President haelewi? kila mtu alieelimika na kuona sehemu zote hapo Tanzania anajua [ukweli] na chaajabu hakuna. Hata hivyo, hakuna hata mmoja aliyejitolea mhanga kusema au kufanya chochote kuzuia hayo madhara. Nyerere pekee ndo alikuwa na kiburi cha kutosha na kusema au kuwa against the big brothers countries. Mr. president tunaomba ucheze fair, politics is a game unatakiwa ucheze kwa uangalifu ama sivyo utachezewa..."[Sadick--U.S]
"...Kama nilivyosema hapo awali sio busara kwa rais wa Tanzania mwenyewe moja kwa moja kujihusisha na malumbano na mtu binafsi. Ni jambo rahisi tu kwa mtu yeyote kuingia kwenye tope na kukwama hata kama mwenyewe hakukusudia. Ndio maana, ni muhimu kutumia vyombo kama Wizara ya Habari, Wizara ya Mambo ya Ndani na kadhalika ili kufikisha ujumbe unaokusudiwa. Kisiasa na kidiplomasia, sio kitu kizuri kwa rais wa nchi kusema kuwa 'ulimi wake umeteleza' pale alipokuwa anaongelea suala fulani, na baadaye kulazimika kufafanua alicho maanisha kwa kauli yake. Ni muhimu kujipatia 'political cover' na 'exit strategy' kwa kuhakikisha kuwa kama rais wa nchi -- because the buck stops at him -- anatunza 'credibility' yake. Acha watu walioko chini waende vitani kwa niaba ya rais, na kama watashindwa basi ndio mzee mzima unakuja baadaye kutoa ufafanuzi, na sio kama jambo hili lilivyofanyika kwa rais kuteleza ulimi wake halafu katibu wa CCM kujaribu kunyoosha lugha. Leo ni suala la filamu ya Darwin's Nightmare, kesho inaweza kuwa suala la ujambazi na kadhalika. Nafikiri wakati umefika wa kujenga institutions zetu mbalimbali na kuzikabidhi kazi ya kujiendesha zenyewe, na vilevile ziweze kujitetea zenyewe. Kama rais ndiye anayekuwa msemaji wetu wa kila kitu, je kuna umuhimu gani wa kuwa na mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa polisi, n.k?..." [ Seppy ]
"..I was impressed by your coverage of the Kikwete's reaction to the movie 'Darwin's Nightmare'..." --[Josiah Kibira, U.S]
"...kimsingi Rais haonekani kama amejiandaa vema katika suala la kuimarisha uchumi wa nchi yetu. Kando na kulumbana na mteng'enezaji wa mshito wa Darwin's nightmare (kazi ambayo pia ingeweza kufanywa na waziri wa Habari), bado Rais haeleweki kakusudia kufanya nini katika kipindi chake cha muhula wa kwanza ili kuinua hali ya uchumi nchini. Na kuhusu suala la siraha, Rais anaweza asijue urasimu unaofanyika huko Mwanza, lakini inaonekana kama kuna ukweli kuhusiana na madai ya Bw. Sauper. Hebu tujiulize, hawa wa-congoleese, Banyamulege, na Ma-savimbi wote silaha wanazitoa wapi? Silaha haziwezi kushuka toka nchi za magharibi kwa miujiza tu, lazima kuna sehemu zinapitia..." [Ed, U.S]
"...Just imagine if someone were to write a critique of some ‘high up'. The next thing you know—treason, sedition, etc. Somehow these ‘bigies' cannot tolerate criticism—and for that reason, they cannot stay away from meddling into the pettiest issues! They cannot tell the difference between art, satire, gutter journalism, or just plain hipe!—Given the amount of attention this issue has generated, we should perhaps not blame him. We do seem bothered likewise this might be in our own image-imago dei!!!...[MK]
"...Mie nafikiri ilikuwa sawa kwa Rais kuingilia kati kwa sababu tuhuma kama za Tanzania kuwa moja ya vituo vya kupakulia silaha kwenye nchi za maziwa makuu ni kitu hatari sana. Ni kitu hatari sana na kinaweza hata kutuharibia uhusiano mzuri tuliokuwa nao na nchi jirani pamoja na international community. Kama unavyojua Tanzania ndio mediator mkubwa wa nchi za maziwa makuu na leo hii tutaonekanaje kama sie tunaonyeshwa ndio wasambazaji silaha ? Tanzania ndio mfano wa amani kwenye bara la Africa je leo tungeonekana vipi kwa kutuhumiwa kuwa tunasambaza silaha na kuchochoea migogoro kwenye nchi za maziwa makuu? Sijui Bwana Hubert Sauper alitoa wapi hizi tuhuma ila inaonekana hazina ukweli wowote. Na nafikiri Rais Kikwete alifanya la maana alipokutana nae na kuuliza hizo evidence lakini tumeona ni majibu gani aliyoyapata toka kwa Bw Hubert Sauper..." [Deusi Gunza, U.S]
"...Hiyo documentary yenyewe mimi sijaiona. Ila huku Musoma na Mwanza watu ni kweli wanakula mapanki..." [James Maziku, Musoma--Tanzania]
"...Salaam zenu wote, I just want to share this information with some of you who may have access to on-demand channel provided by Comcast Cable Network in US. While I was flipping channels yesterday night, I found out you can watch this movie, Darwin's Nightmare, for free. You can search it under category of "Free Movies" at the on-demand channel. It is sponsored by Sundance Channel. I don't know for how long this "pathetic" movie is going to be available for free for all American audience with cable services and some other parts of the world. I doubt if it is only Comcast has listed this movie for free, I guess there could be other cable networks in other areas that are doing the same especially in Europe. It's sad as they have exposed everything under our "kitchen sink" to the rest of the world. To make worse they have even fabricated some scenes to blow some issues out proportion. It's very detrimental for our country especially at this very moment that the country is preparing to start crawling in the global marathon..." [Pius, U.S]
*Makala kuhusu Darwin's nightmare* Kongoli [hapa>>]
Mungu ibariki Tanzania!
Tuma maoni [Hapa>]