JUNZA: SEHEMU YA PILI

Kusikia vile, Junza akamsogelea Lisa kwa karibu na kumpa pliti ya nguvu, pliti iliyomuacha Lisa akiwa ameduwaa kwa dakika kadhaa asiamini alichokishuhudia.

"Lisa nakupenda," Alisema Junza na kuendelea kugonga Ikulu, "Maisha ni kama boksi la chocolate-sikuzote usile krimu yenye ladha ya kahawia kama kwa dhati hutaki."

Basi, alipomaliza kusema hayo, akainuka na kujiondokea zake. Mle chumbani Lisa akabaki ameduwaa. Hakuamini kama Junza angeweza kuonyesha ujasiri wa namna ile mbele zake. Utaalamu wake katika falsafa za maisha ulikuwa umeteka moyo wa Lisa kwa namna isiyoelezeka.

Akiwa amepagawa asijue la kufanya, Lisa akachukua CD nyingine toka kwenye mkoba wake, safari hii ilikuwa CD ya Brandy, na kuanza kucheza wimbo wa 'HAVE YOU EVER?'

Wimbo huu ukazidi kumchagangaya zaidi kiasi cha kumfanya achukue karamu na karatasi na kuanza kuandika maneno yake:-

~~Have you ever loved somebody so much

It makes you cry

Have you ever needed something so bad

You can't sleep at night

Have you ever tried to find the words

But they don't come out right

Have you ever..., Have you ever...~~~

Akaendelea na ubeti wa pili, tatu kisha akamalizia na kibwagizo:-

~~What do I gotta do to get you in my arms baby

What do I gotta say to get your heart

To make you understand how I need you next to me

Gotta get you into my world

'Cuz baby I can't sleep...~~~

Alipomaliza kuandika maneno hayo, akamalizia mwishoni kwa maneno haya:- "Love, Lisa". Baada ya hapo, akaikunja barua ile vizuri kisha akaipulizia perfume kali ya 'Ralph Lauren'. Akiwa njiani kuelekea shule; akapitia dukani na kununua bahasha nyeupe iliyokuwa imechorwa ua la kopa katikati na kuitia barua ile ndani yake.

Alipofika shuleni, akaingia darasani na kuegesha barua ile kwenye dawati la Junza. Lakini kwa bahati mbaya rafiki yake Junza [Brosi] akawa ameshitukia deal na kuichukua barua ile dakika chache baadaye mara baada ya Lisa kuwa ameondoka.

Alipoifungua, akashikwa na butwa! "[Damn!] ina maana Lisa anatoka na Junza?" Haraka akakimbia na kumpasha habari rafiki yake mwingine [Nyankoro]. Nyakoro naye akamtonya Ndekule. Kesho yake habari ikawa imeenea shule nzima. Matroni akapata habari.

Kuona mambo yameharibika, Lisa akavuta kilongalonga chake na kumuita baba yake. "..Baba naumwa". Punde si punde ikaingia shangingi moja ya nguvu pale shuleni na kumkimbiza hospitalini.

Huko hospitalini, madaktari wakashidwa kupata ugonjwa unaomsumbua. Wakaamua kumuita baba yake kwa pembeni na kumtonya, "...Mzee,tatizo liliopo hapa...[pozi], huyu binti anahitaji apatiwe muda wa faragha na kijana wa jinsia tofauti."

[Damn!] Mtihani tihani wa kumpatia binti yake kipenzi muda wa faragha na kijana wa jinsia tofauti ulikuwa mgumu. Kwa kibosile kama yeye asingetaka kusikia masikioni mwake upuuzi wa namna ile. Lakini kwa mapenzi aliyokuwanayo dhidi ya binti yake, akaamua kutii agizo la madaktari.

Wakati anatafakari jinsi gani atakavyotekeleza agizo hilo, akaingia ndani kijana mmoja ambaye hakuwa amevaria vizuri wala kuchana nywele zake.

"Shikamoo mzee," alisikika kijana yule, huku akinyosha mkono kumsalimia babake--Lisa. "Marahabaaaa! Unamfahamu Lisa wewe?," aliuliza mzee yule kwa mshangao!

"Ndiyo," akaendelea kijana yule," actually tunasoma naye B-Academy." Na kabla hajaenda mbali, Lisa akadakizia, "Baba huyu ni rafiki yangu anaitwa Junza, tunasoma nae darasa moja."

Mzee aliposikia, "huyu ni rafiki yangu" machare yakaanza kumcheza. Taratibu akamshika Lisa mkono na kumvuta pembeni huku wakimuacha Junza pekee yake. "Lisa, huyu ni rafiki yako? Ki-vipi? Lisa akakaa kimya. "Naongea na wewe!?" Mzee akanyenyua sauti.

Lisa akavuta pumzi, "Baba najua unaweza usimpende huyu kijana kutokana na mwonekano wake wa nje, lakini huyu mimi ndiye nime....[mpenda]"

Dingi yule aliposikia kuwa binti yake anampenda Junza, akaanza kuponda, "Yaani unampenda huyu kijana!? Akili zako zinakutosha kweli! Kijana gani huyu asiye chana hata nywele!!?"

Kitendo kile kikamuudhi sana Lisa kiasi cha kumfanya aanze kulia, "Ba-ba na-m-pe-nda...," "na-m-pe-nda, jinsi alivyo... [alivyo] "

Aliposikia vile, mdingi yule akaamua kukubaliana na binti yake japo kwa shingo upande. Kikubwa zaidi kilichomfanya akubaliane nae ni suala ambalo daktari alikuwa amemueleza mapema kuwa binti yake alihitaji apatiwe muda wa faragha na kijana wa jinsia tofauti.

"Ok, sweet, uamuzi wako wa kwanza unaweza usiwe sahihi. Nakubaliana na uchaguzi wako. " Akaendelea, "kama kweli mnampenda kwa dhati, mimi sina tatizo. Furaha yako ndio furaha yangu."

Lisa akatabasamu na kuitia kwa sauti ya upole, "sawa baba, nimekusikia."

Baadaye, yalipotimu majira ya jioni, mnene yule akawapakiza kwenye motokari lake la kifahari na kuwapeleka kwenye ukumbi wa starehe wa [LeeBravo] kuwaburudisha. Wakiwa njiani, mdingi yule akachomeka kijembe, "kijana jisikie huru." Kusikia vile, Lisa akacheka na kusema, "Dad!" Kisha akasogea kwenye siti ya Junza na kupitisha mkono juu ya mabega yake, "dingi anapenda sana jokes naomba usi-mind bana. "

Wakiwa mwendo wa dakika kumi tu kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa starehe wa LeeBravo, taili la mbele la gari likachomoka. Gari ikaanza kuyumba huku na kule huku dereva asijue la kufanya. Mbele yao kulikuwa na Lori la mizigo, na pembeni kulikuwa na watoto wadogo wakicheza chandimu. Gari ikazidi kuserereka huku ikiyumba kwa nguvu. [Vupu!!!!] Ghafla ukasikika mlio mkubwa. Maskini! Gari alilokuwemo Lisa pamoja na Junza lilikuwa limegonga na kuingia uvunguni mwa Lori la mizigo lililkuwa mbele yao.

Usukani wa gari ulikuwa umechomoka na kumbana babake--Lisa kifuani na kumuua paleple! Junza pamoja na Lisa walikuwa wameumia vibaya sana! Wote wawili walikuwa wamepoteza fahamu.

Muda si muda, Ambulance ikawakimbiza hospitalini kwa ajili ya matibabu ya haraka. Walipofika Hosptalini madaktari wakagudumua kuwa Lisa alikuwa amepoteza damu nyingi sana. Mshipa mkuu wa damu ulikuwa umepasuka na kuvujisha damu kwa ndani. Jeraha kubwa alilokuwa nalo kichwani pia lilikuwa limesababisha damu kuvujia ubongoni kwa wingi.

Nusu saa tu baada ya kuwa amelazwa hospitalini, Lisa akavuta pumzi yake ya mwisho na kukata roho . [Masikini!]

Kwa upande wa Junza, yeye alikuwa mahututi zaidi. Ikabidi madaktari walazimike kumfungia vifaa maalum vya kumsaidia kupumua. Madaktari wakapigana kiume wakifanya kila wawezalo ili kuyanusuru maisha yake lakini kadri mshare wa saa ulivyokuwa ukizidi kusogea mbele, ndivyo hali ya Junza ilivyozidi kuwa mbaya.

Na ilipotimu saa tano na robo usiku, Junza naye akavuta pumzi yake ya mwisho na kukata roho bila hata ya kupata fursa ya kufurahia bahati ya kupendwa na mtoto mrembo wa kimanga!

Kwenye mazishi; Padre aliyeendesha misa, alinukuu maneno yaliyowahi kusemwa na mwana-falsafa mmoja wa karne ya kumi na tisa kwa kusema, "Maisha ni mafupi, na hatuna muda mwingi wa kufurahisha nyoyo za wale tunaosafiri nao katika dunia hii yenye kiza. Uwe mwepesi basi wa kupenda! Fanya haraka kuwa mwema kwa wenzako."

**MWISHO**

©copyright:- BongoTz.Com MMVI.

<<BACK TO MAIN PAGE >>

©Copyright:BongoTz.Com -MMV. All Rights Reserved.