April 23, 2010

 

 

MWAFRIKA, NANI "DADDY" YAKO ?

Ajabu sana,!! kila siku utasikia watu Afrika wakipayuka, “…oh vijana wa siku hizi wamepotoka, wanaiga Tamaduni za kigeni, wanavaa nguo za ajabu, blaaa, blaaa...” Kitu kimoja najiuliza, hivi Tamaduni asili ya mwafrika ni ipi? Ni nini mavazi asilia ya mwafrika? Ni nini muziki asilia wa mwafrika? Ni nini lugha asilia ya mwafrika? Ni nini dini asilia ya mwafrika? Zaidi ya maswali 67 bila majibu. Kama kawaida na desturi za kiafrika, hivi karibuni niliamua kutafuta majibu ya maswali haya kutoka kwa mababu na wazee waheshimiwa katika sehemu ya Afrika niliyozaliwa iitwayo Tanzania. . [Habari Kamili>]

DARWIN'S NIGHTMARE: JE, KUNA UKWELI NDANI YAKE?

Gazeti la kila siku la kiswahili, Alasiri [01, August, 2006] lilichapa habari iliyokuwa na kichwa "Rais kufa na mtu" na kuelezea jinsi Rais Kikwete alivyo kasirishwa na tuhuma nzito ndani ya mshito (documentary) ya Darwin's Nightmare iliyoteng'enezwa na mzungu Hubert Sauper mzaliwa wa Austria aishiye Ufaransa. Rais, alikaririwa akidai kuwa madai ya Bw. Sauper yalikuwa ya kizushi na yasiyo na ukweli wowote ndani yake. Lakini kwa uchunguzi uliofanywa na tovuti hii, madai ya Bw. Sauper huenda yana ukweli fulani ndani yake. ...[Habari Kamili>]

JE, KIKWETE ANASTAHILI SIFA ZOTE HIZI?

Ni ukweli usiopingika kwamba Tanzania ina utajiri wa kutosha na inaweza kabisa kufanya vizuri zaidi ya kukurukakara za hapa na pale za kupapasa mambo madogo-madogo zinazofanywa na serikali ya awamu ya Nne. Tatizo ni kwamba, kama wananchi wenyewe wamelemazwa na kauli mbiu ya "...nguvu, kasi na ari mpya," watawezaje kuamka na kugundua kuwa kauli hizo ni kelele tupu zisizolipeleka taifa lete popote pale...!? Utajiri wa Tanzania hauishii kwenye madini na utalii tu, kuna vitu vingine vingi kama vile hekari millioni 44 za misitu (Lakini shule hazina madawati!), ziwa kubwa barani Afrika (Victoria) lililojaa kila aina ya samaki (Sangara kwa mfano, ambao wengi wanaishia Ulaya chini ya mikataba mibovu) , gesi za asili (songosongo) , bandari kuu nne za Dar-es-salaam, Tanga, Zanzibari na Mtwara lakini bado bajeti ya Taifa tunategemea nchi wahisani!? Bado serikali haiwezi kuboresha miundombinu? Bado Hospitali nchini hazina vitanda wala madawa ya kawaida kama Aspirini? Bado Tanzania ni ya tano toka mwisho kwa uchumi duniani?....[Habari kamili >>]

©Copyright: BongoTz.Com-MMV. All Rights Reserved