SEHEMU YA- III

Kapteni akacheka na kusema: "Well...," na kabla hajamalizia kusema anchotaka kusema, Shenene akamkata na kusema, "nataka tufanye mapenzi sasa hivi tena hapa hapa."

Lakini Kapteni akakataa katakata. "Shenene,sidhani kama hilo ni wazo zuri.Wewe hunijui,mimi nae sikujui--tumekutana jana tu!... Kwanini tusilipatie hili jambo muda kama kweli unania na mimi." Kapteni akasisitiza.

Kusika vile,Shenene akatikisa kichwa na kubonga ung'eng'e,"So,you think this is love in the first place-huh!?!" Akahoji na kuendelea,"No!, it's not!...I never dreamed to meet someone gentle,considerate,and humble like you [ Mhhhh-akakwamwa na sauti ]....And don't think that I'm just a simple girl who is desperate for the love at the first time...I'm not Kapteni!--I love you!" Akalia na kutoka nje ya ukumbi.

Basi Kapteni akawa hana budi kuyatekeleza yale aliyoyatamka Shenene.Lakini moyoni akawa ana sita na kujiuliza,"Idon't think so...this is to good too be true."

Shenene akaingia ndani ya motokari yake na kujiraza kwenye siti ya nyuma,huku akilia kwa uchungu wa kukataliwa na mtu ambaye hakuwa wa hadhi yake.

Ghafla akasikia mtu anapapasa kioo cha gari...akanyenyua kichwa juu kutaka kujua ni nani. [Lo!] Kuona vile, akaharakisha kufuta machozi ili Kapteni asigundue kuwa alikuwa analia.Baada ya kufuta machozi,akafungua mlango wa gari na kumruhusu Kapteni kuingia ndani.

"Wow!! ,"Kapteni akapigwa na bumbuwazi...."Shusha nguo yako chini kidogo,naniii yako inaonekana..." [ akachindwa kusema chupi ]yako inaoneka.]

Ingawa alikuwa na hasira moyoni;Shenene akashidwa kujizuia--mara akajikuta ana tokwa na tabasamu. Kwa sauti ya chini akarusha kijembe,"Palipo na maji tele...,wajinga hufaa kwa kiu..."

"Ha,ha,ha..." Kapteni akacheka na kusema,"...pia mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani."Akamuacha Shenene solemba--asijue Kapteni kamaanisha nini.

"Damn!,this dude is smart." Shenene akajisemea moyoni.

Wakiwa mle ndani ya gari,Shenene akataka kutumia kila aina ya mbinu kumnasa Kapteni. "Humu ndani kuna joto," Shenene akasema huku akisaulasaula kivazi chake.

"Shenene!, unafanya nini hicho...!?" Kapteni akahoji kwa mshangao! "Nimekwambia nasikia joto..."Akajibu mrembo yule huku akiyalembua macho yake mazuri.

Dakika hazikupita,Kapteni akajikuta anatizamana ana kwa ana na bikini za rangi ya kahawia [damn!]. Ugumu wake wote ukaanza kuyeyuka taratibu mithili ya bonge la barafu lililoachwa juani kwa muda mrefu.

"Kapteni, naomba unipatie massage mgongoni. Najisikia niko very stressed-up." Akajilaza kwenye siti ya nyuma huku mrindimo wake ukijitokeza kwa juu utadhani kilele cha mlima kilimanjaro.

[Kimya! ]--Kapteni alikuwa hata hasikii alichokuwa akielezwa na Shenene,mawazo yake yalikuwa yamechotwa na umbile nzuri la binti Stadmire.

"Kapteni...," akaita tena kwa sauti nyororo huku akitabasamu kwa maringo na majivuno. "Please,I need massage..." Shenene akazidi kusisitiza.

"Oh, massage...poa--haisumbui." Kapteni akaitikia na kumsogelea kwa karibu. "Una mafuta yoyote ya lotion humu ndani...?"-akauliza. Shenene akageuka na kusema,"Angalia kwenye mkoba wangu, kuna kichupa kidogo kilichoandikwa--Aloe Vera lotion."

Kapteni akakichukua na kumimina lotion kidogo mkononi kwake kisha akaanza shughuli.

"Mhhhh.., mhhhh..., mhhhhh.....,Ohhhh...,it feels so good Kapteni" Shenene akawa analalamika kadiri mikono migumu iliyogangamala ilivyokuwa inazidi kuteng'eneza mawimbi mgongoni mwake kwa madaha na ufundi wa hali ya juu.

"Do you like it...?" Kapteni aliuliza.

"Oh, yes honey...keep doing it... don't stop..." Shenene akaitikia kwa sauti laini ya mahaba.

Taratibu Shenene akaanza kupandwa na mwashawasha ...

SEHEMU YA -IV

"Mhhh....Mhhh...Mhhh..., Kapteni; umejifunzia wapi haya mambo jamani...?," aliuliza shenene kwa sauti nyororo na tulivu huku akishindwa kuunganisha maneno vizuri.

Kapteni akatabasamu na kusema, "Well,ex-girlfriend wangu alikuwa anapenda sana massage...kwake massage ilikuwa kama desturi--alikuwa hawezi kupata usingizi bila kupewa massage."

Kusikia vile, Shenene akamgeukia Kapteni na kuhoji, " eeh, ilikuwa-kuwaje mpaka mka-break up?"

"No,no.No.Stop!--tafadhali naomba usinikumbushe!" Kapteni alisihi.

"Hey, I'm so sorry for what happened between you and your ex..., " Shenene akakoroga kimombo na kuendelea, "It's alright, take it easy,I've been there too rafiki!"

Kusikia vile, Kapteni akafarijika na kujisemea moyoni --oh,kumbe siko mwenyewe katika ulimwengu huu wa kukataliwa. "Alright, nitakuelezea ilivyokuwa...," Kapteni akajitutumua.

"Mimi na Twikishi tulikutana kipindi tukiwa O-level..., na siku ya kwanza tu nilipomtia jicho nilijua moyoni kuwa-huyu ndo' mwenyewe. Basi,nikamuomba awe rafiki yangu naye akakubali. Haukupita muda--sote tukawa tumezama katika dimbwi zito la mapenzi..."

"Eeh...,endelea..," Shenene akadakiza kwa sauti laini iliyosuzika.

"Basi bwana, kwa muda wote tuliokuwa O-level [form I-form-IV], tukajiona kuwa sisi ni yote katika yote [invincible] .Hatukuona kama kuna kitu chochote kinakachoweza kututenga..,.na muda si muda -tukamaliza kidato cha nne."

"Wow!," Shenene akashingwa na mshangao! "...and what happened next?" Shenene akahoji.

"Well, mimi nilifaulu kwenda Tambaza na Twikishi akafeli mtihani. Yeye alipata division four na kukosa nafasi ya kujinga na kidato cha tano.Hilo likawa limemchangaya akili sana kwasababu alikuwa mtu aliyependa sana shule. Nahisi kilichomuumiza zaidi ni maneno ya watu mitaani. Maana kila alipokatiza, alipigwa madongo makali kama- 'huyo...kanogewa na penzi kiasi cha kusahau kilichompeleka shule...,muone...,kadunda sasa...,Ovyo...!'

"Kapteni, hudhani kwamba wewe ulichangia kwa kiwango kikubwa ktk kufeli kwake?" Shenene akadakizia.

"Oh, no. No!, "Kapteni akatikisa kichwa na kukataa katakata,"haikuwa bahati yake tu."

Baya zaidi, mama yake alipopata habari kuwa nilikuwa natembea na binti yake,nasikia akawaka ile mbaya--yaani kinoma! Akamugombeza na kumwambia, "zero wewe...yaani nimepoteza hela zangu nyingi,kumbe ulichokuwa unakifanya huko shuleni ni kuwapanuliwa wavulana mapaja tu...,funga virago vyako..., funga na ondoka hapa kwangu! Nenda hukohuko kwa hao waume zako...,malaya mkubwa wewe!" Kitendo kile kikamuudhi sana Twikishi.Basi akaenda dukani akanunua klorokwini 30 na kuzibwia..., nyuma akaacha barua iliyokuwa inaelezea kwanini ameamua kuondoa uhai wake."

"Barua yenyewe ilikuwa inasemaje?," Shenene akauliza.

"Well, kifupi alinitaja mimi kuwa chanzo cha yeye kufeli...kitu ambacho hadi leo sikubaliani naye kabisa! Kwasababu kama mimi ndiye niliyesababisha yeye kufeli, mbona mitihani yake ya kawaida [darasani] alikuwa anafanya vizuri?" Alihoji Kapteni.

"Kwakweli-baada ya Twikishi kujiua binafsi iliniumiza sana na kunifanya niachane kabisa na mambo ya wasichana." Kapteni alimalizia huku machozi yakimdondoka usoni.

"Pole sana kwa yote hayo!" Shenene akampoza na kuendelea,"ni vizuri zaidi kujutia kitu ulichofanya kuliko kitu ambacho hukufanya..., binafsi,sioni kwanini ujutie jambo ambalo kwa dhati unafahamu fika kuwa hukufanya..."Shenene alizidi kugonga ikulu.

"Naomba unisikilize kwa makini Kapteni," akaendelea "una kitu cha thamani ndani yako ambacho wengi wangetamani kujiua ili wakipate."

"What do you mean?" Kapteni akauliza kwa ukali.

"I mean, ustaarabu.Unajua ustaarabu hauna gharama yoyote ile na unanunua kila kitu."[pozi] "...Maishani mwangu sijawahi kumweleza mvulana kuwa na-m-pe-nda,lakini leo naomba nikwambie waziwazi kuwa na-ku-pe-nda,na sababu kubwa inayonifanya nikupenda ni--ustaarabu wako." [kimya] "....nafahamu kuwa mtu akishaumwa na nyoka ,akiguswa na unyasi anashtuka..., hilo nalielewa vema Kapteni! Lakini kwangu mimi--It doesn't matter what you've been through;where you came from;who your parents are or what your social or economical status is.None of that matters to me. What matters to me is- 'I love you for who you are' and I want to be in your life.Period! So, think of it and tell me now if you're for it or against it...

KUSOMA SHEMU INAYOFUATA: [Kongoli hapa>>]

 

©Copyright:BongoTz.Com -MMV. All Rights Reserved.